Mwanamume mmoja raia wa Marekani anashukiwa
kuwaua watoto wake watano na kuwatupa katika jimbo jingine, hii ni kwa
muujibu wa polisi nchini humo. Timothy Ray Jones anakabiliwa na
mashtaka kadhaa katika jimbo ambalo ndio makazi yake la Carolina ya
kusini,kufuatia shutuma hizo na alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita
huko Mississippi .
Watoto hao watano waliopoteza uhai kwa kuuawa
na baba yao walikua na umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi miaka nane
inaelezwa watoto hao watano walipotea katika mazingira ya kutatanisha ,
mama wa watoto hao aliporipoti polisi baada ya mawasiliano kati yake na
mzazi mwenziwe kukatika.
Maafisa hao wa polisi walipofanya
uchunguzi wao waligundua miili ya watoto hao imezikwa karibu na mji wa
Alabama karibu na barabara kuu baada ya kuwasaka watoto hao kwa siku
nzima .
Jones alisimamishwa katika kizuizi cha barabarani na
kushukiwa kua alikua akiendesha gari baada ya kutumia dawa za kulevya
,imethibitika kuwa katika gari yake kulikuwa na kemikali zinazoaminika
kua dawa za kulevya, zaidi ya hapo polisi walikuta damu garini mwake na
alikua akitafutwa huko Carolina ya kusini .
Kitengo
kinachoshulikia usalama wa raia huko Alabama kimesema kupitia kwa
msemaji wake sajenti Steve Jarrett kwamba baada ya msako huo Jones baba
wa watoto hao aliwaongoza maafisa hao hadi eneo alikozika miili ya
wanawe.
0 comments:
Chapisha Maoni