Ili kuongeza utendaji kazi wa walimu Chama cha walimu Mkoani Iringa kimeitaka serikali kuwalipa madai ya madeni yao kwa wakati na kutopunguza malipo ya mafao ya hifadhi za jamii.
Katibu wa chama cha walimu Mkoani Iringa Bw.Mshamu Muhamed amesema tangu January mwaka huu vimefanyika vikao vingi kati ya viongozi wa CWT kitaifa na wizara ya elimu pamoja na kamati ya utumishi ambapo utekelezaji wa madai yao bado haujafanyika.
Bw.Muhamed ameongeza kuwa deni la CWT kwa serikali kitaifa ni zaidi ya tilioni tano na kwa mkoa wa Iringa pekee ni zaidi ya milioni 871 ambazo ni zinatokana na kutolipwa kwa ghalama za uhamisho,semina na mafunzo mbaimbali pamoja na kutolipwa kwa mshahara kulingana na dalaja husika.
Naye Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Iringa Bw.Stanslaus Mhongole amesema licha ya serikali kuwa na limbikizo kubwa kwa deni la walimu,chama hicho hakiungi mkono mpango wa serikali wa kupunguza malipo ya mafao ya hifadhi za jamii.
Hata hivyo Bw.Mhongole amesema tamko lao ni la wiki mbili hivyo amewataka walimu wa halmashauri zote Mkoani Iringa waweze kuwasilisha madai yao kwa maafisa elimu ili baada ya tamko waweze kumfuata Mkurugenzi wa mkoa.

0 comments:
Chapisha Maoni