Mtoto wa miaka miwili aliyefahamika kwa jina la Grolia Levocatus mkazi wa Itewe amefariki baada ya kugongwa na gari ambalo halikufahamika maramoja ambalo pia lilikuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika kwa jina wala anuani yake.
Ajali hiyo imetokea jioni ya juzi saa moja na nusu huko Itewe katika wilaya ya Mbalizi mkoani hapa Mbeya katika barabara ya Mbeya-Iringa huku chanzo cha ajali kikiwa bado hakijafahamika na bado jeshi la polisi linachunguza juu ya kutikea kwa tukio hilo.
Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya lakini imefahamika pia kuwa dereva wa gari lililosababisha kifo hicho alikimbia baada tu ya tukio japokuwa bado jeshi la polisi linamsaka.
Akiithibitishia Fichuo Tz juu ya kutokea kwa tukio hili kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi ametoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto kwa kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.



0 comments:
Chapisha Maoni