KAMPUNI ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na wadai wengine wawili wamefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na wengine watatu wakitaka kulipwa fidia ya sh. bilioni 500 kwa kashfa alizotoa kimaandishi dhidi yao.
IPTL pia ilishamfungulia Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ikimtaka kuomba radhi na alipe shilingi bilioni 310 kwa kuidhalilisha kampuni hiyo.
Mbali na IPTL, wengine waliofungua kesi hiyo Septemba 4, kupitia wakili Melchisedeck Lutema wa Asyla Attorneys na Kay Felician Mwesiga wa Bulwark Associates Advocates, ni kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo, Harbinder Sing Seth.
Wadai hao watatu, miongoni mwa mambo mengine wanahitaji malipo ya fedha kutoka kwa Zitto na washtakiwa wengine watatu ambao ni Mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Kampuni ya Raia Mwema na kampuni ya Flint Graphics, kuwa kama fidia itokanayo na makala ya kuwachafua iliyochapishwa kwenye gazeti hilo, iliyosababishwa na washitakiwa hao.
Pamoja na hayo, pia wanahitaji tamko rasmi toka mahakamani kwamba makala iliyokuwa na kichwa cha habari “Fedha za IPTL ni mali ya umma” iliyochapishwa katika kurasa wa 7 na 14 za gazeti la Agosti 13, 2014 ilikuwa ni ya kupotosha na kuchafua kwa kudhamiria na kuhitaji washitakiwa kuomba radhi.

0 comments:
Chapisha Maoni