Watu wanne wamepoteza maisha yao katika
ajali ya barabarani mkoani Mbeya huko wilayani Kyela baada ya magari
mawili kugongana majira ya saa moja jioni katika maeneo ya Utengule
katika jia ya Mbeya-Tukuyu.
Maafisa wa polisi wamewataja
waliokutwa na mauti katika ajali hiyo kuwa ni Mortina mwenye miaka 30,
Edina Jackson mwenye miaka 22, Paulo Mwanyalila ambaye ni Padri wa
kanisa la Roman Catholic Kyela pamoja na mwanamke ambaye hakuweza
fahamika jina.
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi dogo
aina yaToyota Coaster iliyosajiliwa kwa namba T. 241 BKZ lililokuwa
likiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika mara moja na gari ya pili ni
ambalo halikufahamika ambapo baada ya kutokea tukio hilo watu wengine
watatu walijeruhiwa ambao ni Samweli Asanga mwenye miaka 34, Mawazo
Gasper pamoja na mtoto wa miaka kati ya 2-3 ambaye hakufahamika jina
lake na madereva wote walikibia baada ya kusababisha ajali.
Chanzo
cha ajali hiyo bado hakijafahamika na kinachunguzwa. Miili ya marehemu
imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya na majeruhi pia wamelazwa
hospitalini hapo.



0 comments:
Chapisha Maoni