Bwana mmjoja aliyefahamika kwa jina la Levis Mlenga aliye na miaka 43 mkazi wa Lufita, Malawi amefariki dunia akiwa amefungiwa ndani ya chumba cha ofisi ya kata baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kusadikika kuwa ameiba ng'ombe wawili wa Emmanuel Kilembe mkazi wa kijiji cha Ilondo. Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Fichuo Tz kuwa tuko hilo lilitokea usiku wa kuamkia siku ya jumamosi iliyopita kijijini Malangali,Ileje mkoani Mbeya baada ya marehemu kukamatwa askari polisi kutoka nchini Malawi na alipojaribu kuroka ndipo akashambuliwa na wananchi kitu kilichopelekea avuje damu nyingi puani na mdomoni.
Kufuatia tukio hilo watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi. Watu hao ni Emmanuel Kilembe, Itison Ndimbwa na Furaha Kibona ambaye ni kaimu mtendaji wa kata ya Malangali.
Kufuatia tukio hilo watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi. Watu hao ni Emmanuel Kilembe, Itison Ndimbwa na Furaha Kibona ambaye ni kaimu mtendaji wa kata ya Malangali.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Itumba.
Kamanda wa polisi mkoa wa MBEYA, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na na kuwataka wanchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.




0 comments:
Chapisha Maoni