Jumatatu, Septemba 15, 2014

PAPA FRANCIS ATABIRI VITA KUU YA TATU YA DUNIA

Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametahadharisha juu ya kuongezeka machafuko na mapigano na kusisitiza kwamba ulimwengu unanyemelewa taratibu na Vita vya Tatu vya Dunia. 
Akizungumza kwenye maadhimisho ya kukumbuka kutimia miaka 100 tokea vilipoanza Vita vya Kwanza vya Dunia, Papa Francis amesisitiza kuwa, taratibu Vita vya Tatu vya Dunia vinaunyemelea ulimwengu, kwani kiwango cha jinai, mauaji, ukatili na uharibifu duniani kimeongezeka mno. 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amewataka walimwengu kuzingatia suala hilo na kuongeza kuwa, leo hii wahanga wamekuwa wengi mno, na kuhoji vipi linawezekana kutokea jambo kama hilo? 
Kiongozi huyo wa kiroho amesema kuwa, sababu kuu ya ulimwengu kugubikwa na machafuko na migogoro ni kutokana na baadhi ya viongozi kupenda kuhodhi madaraka na kupora mali. 
Papa Francis ametaka yakomeshwe haraka mapigano yanayoendelea huko Ukraine, Mashariki ya Kati na maeneo mengine duniani.

0 comments:

Chapisha Maoni