Ndege ya kivita ya Nigeria imetoweka katika operesheni dhidi ya
wanamgambo wa kitakfiri wa Boko Haram katika eneo lililoathiriwa na
machafuko la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Nigeria imeeleza kuwa ndege hiyo ya kivita
ilitoweka ikiwa na marubani wawili. Msemaji wa jeshi la Nigeria Meja
Jenerali Chris Olukolade amesema kuwa ndege hiyo iliyotengenezwa
Ujerumani, Ijumaa iliyopita iliondoka katika kituo cha kijeshi cha Yola
makao makuu ya jimbo la Adamawa kwa ajili ya operesheni ya dakika 75.
Amesema tangu siku hiyo mawasiliano na ndege hiyo yamekatika.
Jeshi la Nigeria limekuwa likitumia ndege za kivita kuyashambulia
maeneo ya wanamgambo wa Boko Haram. Msemaji wa jeshi la Nigeria
ameongeza kuwa juhudi za kuwasiliana na marubani wawili wa ndege
iliyotoweka bado zinaendelea.
0 comments:
Chapisha Maoni