Alhamisi, Septemba 04, 2014

LEO BEYONCE KNOWLES ANATIMIZA MIAKA 33, MAMBO YAKE MENGI USIYOYAJUA YAKO HAPA

Siku kama ya leo septemba04, 1981 ndio siku aliyozaliwa staa wa muziki Beyonce knowles katika mji wa Texas kwahiyo anatimiza miaka 33.
Beyonce Knowles kabla ya sasa aliwahi kuwa mmoja wa wanamuziki katika kundi la Destiny Childs na baadaye akafanikiwa kuwa mwanamuziki maarufu bila ya kundi yaani 'Solo Artist'. Alishinda tuzo za Grammy Award mwaka 2013 akiwa na miaka 17 tu, ambapo wimbo wake "Love on Top" uliposhinda katika kipengele cha 'Best Traditional R&B Performance'. Kabla hajawa staa Beyonce aliwahi kushinda tuzo yake ya kwanza katika tamasha la shule aliyokuwa akisoma baada ya kuperforme wimbo uitwao "Imagine" ambao uliimbwa na John Lennon. Pamoja na hayo mbali na Beyonce kuwa staa wa muziki pia alianza kushiriki katika filamu ambapo filamu yake ya kwanza ni Dreamgirls, ambayo ilimkutanisha na mastaa wengine akiwepo Eddie Murphy na Jennifer Hudson. Beyonce ameolewa na Jay-Z tangu Aprili 4, 2008 ana tayari ndoa yao imezaa matunda ya mtoto mmoja aitwaye Blue Ivy aliyezaliwa mwaka 2012. Pia Beyonce anaye dada anaitwa Solange na kaka yake Nixon.

0 comments:

Chapisha Maoni