Alhamisi, Septemba 11, 2014

HILI KUWA MKOMBOZI WA GHARAMA ZA AFYA IRINGA

Ili kuondokana na ghalama na kupata matibabu kwa wakati wananchi Mkoani Iringa wametakiwa kutumia mfumo mpya wa matibabu wa tiba kwa kadi. Mganga Mkuu wa Afya Manispaa ya Iringa Dkt.May Alexander amesema mfumo huo wa tiba kwa kadi unatumika kwenye zahanati na vituo vya afya vyote vya manispaa ya Iringa ambapo ghalama ya kujiunga na kadi hiyo ni shilingi elfu kumi ambayo itatumika kwa mwaka mzima.
Dkt.Alexander ameongeza kuwa theluthi mbili ya kiasi cha fedha hiyo hutumika katika manunuzi ya madawa na kiasi kinachobaki hutumika kwa ajili ya maboresho ya majengo na malipo kwa walinzi hali ambayo hupelekea upatikanaji wa dawa na vifaa mbalimbali vya matibabu.
Naye Muuguzi wa Hospitari ya Frelimo Manispaa ya Iringa Bi.Anna Kiyagi amewataka wananchi kujiunga katika mfumo huo kwani hali ngumu ya maisha husababisha baadhi ya wagonjwa kushindwa kughalamia matibabu hali inayopelekea vifo.
Hata hivyo Mganga Mkuu wa Afya Manispaa ya Iringa Dkt.Alexander amesema mfumo huo unatumika ndani ya Manispaa ambapo halmashauri zote za Mkoa wa Iringa zinatumia mfumo wa CHF pia wapo katika mpango wa kuiingiza hospitari ya Mkoa wa Iringa iweze kutoa huduma za matibabu kwa mfumo wa tiba kwa kadi.

0 comments:

Chapisha Maoni