Alhamisi, Septemba 11, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Siku kama ya leo miaka 331 iliyopita, inayosadifiana na 12 Septemba 1683, vita vikali kati ya utawala wa Othmania na vikosi vya majeshi ya Austria na Poland vilishadidi, baada ya majeshi ya utawala wa Kiothmania kusonga mbele na kuwa na satua zaidi huko Ulaya. Katika kipindi hicho, ilikuwa imepita karibu miezi miwili tokea jeshi la Othmania lilipofanikiwa kuuzingira Vienna, mji mkuu wa Austria, suala ambalo lilizitia wasiwasi mkubwa tawala za Ulaya juu ya kuandaliwa mazingira ya kupata nguvu utawala huo huko Ulaya 
Siku kama ya leo miaka 37 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 12 Septemba 1977, alifariki dunia Steve Biko mwanaharakati wa kupigania haki za wazalendo wa Afrika Kusini, akiwa chini ya ulinzi wa polisi. Steve Biko alikuwa kiongozi wa wanafunzi aliyefanya jitihada kubwa za kuwawezesha wazalendo waliokuwa wakibaguliwa wa Afrika Kusini na kuratibu harakati zao. Baada ya kufariki dunia akiwa mikononi mwa polisi, Biko alitambuliwa kuwa shahidi wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi. Alikuwa mashuhuri kwa kaulimbiu ya "Weusi ni Uzuri" (black is beautiful) ambayo ililenga kuwapa moyo wazalendo wa Afrika Kusini waliokuwa wakibaguliwa kwa sababu ya rangi ya ngozi yao.
Tarehe 12 Septemba 1944, wawakilishi wa Marekani, Uingereza na Urusi walitia saini makubaliano ya kuikalia kwa mabavu Ujerumani wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Utawala wa Kinazi wa Ujerumani ulisambaratishwa kikamilifu mwezi Mei 1945, na kudhibitiwa kikamilifu mji wa Berlin baada ya kutokea mashambulizi yaliyofanywa na majeshi ya waitifaki wa Magharibi na Mashariki. Hatimaye mwaka 1949 nchi hiyo ilizidi kutumbukia kwenye mkwamo baada ya kugawanyika nchi mbili za Ujerumani ya Magharibi na Mashariki.
Na siku kama ya leo miaka 117 iliyopita, inayosadifiana na 12 Septemba 1897, Irene Joliot- Curie mtaalamu wa fizikia na kemia wa Ufaransa, alizaliwa katika mji wa Paris. Baada ya kufanya utafiti wa muda mrefu, Irene Joliot- Curie alifanikiwa kuvumbua mada za radioactive.

0 comments:

Chapisha Maoni