Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya baada ya kukamatwa na pombe haramu ya moshi (Gongo) kiasi cha lita 10 katika maeneo ya Soweto, jijini Mbeya.
Jeshi la polisi limesema kuwa watu hao wanaoshikiliwa na jeshi lao ni Oliva Lugano mwenye miaka 22, ni mkazi wa Soweto, Asha Simba mwenye miaka 25 anayeishi Juhudi na Evelina Simonaliye na miaka 23 mkazi wa Kagera, maeneo yote yanapatikana jijini Mbeya.
Watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa nne asubuhi baada ya kufanyika msako katika maeneo ya Soweto kata ya Ilomba na Tarafa ya Iyunga. Kiasi hicho cha gongo kilikutwa ndani ya nyumba ya wanamoishi watuhumiwa mara baada ya kupekuliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni