Waziri wa Afya wa Senegal amethibitisha kua ugonjwa
wa Ebola umekwisha tua nchini mwake na kufanya hesabu ya kua nchi ya
kumi na tano kutoka Africa magharibi kukumbwa na ugonjwa huo .
Mwishoni mwa wiki waziri huyo Awa Marie Coll
Seck aliwaambia waandishi habari kwamba kijana mmoja kutoka Guinea
aliingia nchini Senegal akiwa ameshaambukizwa ugonjwa wa Ebola, na
alipogunduliwa, mara moja aliwekwa katika karantini.
Mripuko wa hivi karibuni ulitokea nchini Guinea, umeua Zaidi ya watu 1,500 .
Na wengine 3,000 waliambukizwa virusi vya
ugonjwa huo nalo shirika la afya duniani limeonya kua hali inaweza kuwa
mbaya Zaidi na huenda ukaambukiza watu wengine Zaidi ya 20,000 people.
Kutokana na kutambuliwa kwa mgonjwa huyo Senegal
imefunga mipaka yake na nchi ya Guinea ili kuepusha kuenea zaidi kwa
ugonjwa huo.
0 comments:
Chapisha Maoni