Baada ya Mbeya City kurejea kutoka Mikoa ya Rukwa na
Katavi kusaka vipaji na makali ya Ligi Kuu Tanzania bara, ndugu zao
Tanzania Prisons wanondoka leo kwenda Mjini Sumbwanga kwa mechi za
kirafiki.
Kwa mujibu wa Meneja wa timu hiyo, Enock Lupwuto, wanakwenda mjini
Sumbawanga Mkoani Rukwa kwa mwaliko wa Chama cha Soka Mkoa huo
(RUREFA) ambako watajifua kwa kucheza mechi za kirafiki.
Akizungumza na Fichuo Tz , Meneja huyo alisema safari
ilianza jana majira ya asubuhi kwa basi la timu hiyo na wakiwa mjini
Sumbawanga, watacheza mechi mbili ya kwanza itakuwa dhidi ya Kombaini
FC mchezo ambao utapigwa leo katika dimba la Nelsoni Mandela.
Lupwuto alisema kuwa, mbali ya mechi ya leo timu hiyo itashuka
dimbani Jumapili dhidi ya timu watakayopangiwa na wenyeji wao ambao
ni chama cha soka Mkoa wa Rukwa.
Aliongeza kuwa, baada ya timu yao kufanya vibaya katika msimu
uliopita ambapo ilimaliza ikiwa nafasi ya kumi na moja, safari hiii
wamedhamiria kufanya vizuri zaidi ikiwa ni kutwaa ubingwa msimu.
Tanzania Prisons iliyopanda daraja mwaka 1995 na kuwika vilivyo
katika soka ya Tanzania hadi kuwahi kucheza michuano ya kimataifa,
itaendoka leo ikiwa na wachezaji 27 na viongozi watano ambapo
watarejea jiji Mbeya Semtemba mosi.
Alisema baada ya kurejea jiji Mbeya, Semptemba 3 msafara wa timu
hiyo utaondoka kuelekea jiji Dar es Salaam kucheza mechi kadhaa za
kirafiki kabla ya kuanza kwa kampeni ya Ligi Kuu itakayoanza Semptemba
20.
Tanzania Prisons inayonolewa na Devid Mwamwaja inafanya ziara
hiyo ikiwa ni siku kadhaa tangu wawakilishi wengine kutoka Mbeya,
Mbeya Cit FC kurejea kutoka katika ziara ya mkoa wa Rukwa na Katavi
ambako mabli ya mechi za kirafiki, waliitumia fursa hiyo kufungua
matawi.
0 comments:
Chapisha Maoni