Kikundi kimoja cha kujitolea nchini India kimegawa
vyoo 108 bure katika kijiji ambako wasichana waliuawa kwa kunyongwa
katika miti mwezi mei mwaka huu
Wasicha watatu wapwa waliuwa katika eneo la Katra Sahadatganj huko Uttar Pradesh wakati walipokwenda kujisaidia porini.
Wanaharakati waliliona hilo la uhaba wa vyoo
ambalo liliwalazimu wasicha na wanawake kutembea umbali mrefu ili
kujisaidia na ndiko huko hukumbwa na masahibu.
Nusu ya watu nchini India sawa na watu bilioni 1.2 hawana vyoo vya kujihifadhi.
Na wakasema kufuatia vyoo hivyo nafuu wanaamini
hakuna mwanamke ambaye atapoteza uhai ati tu kaenda haja.ni kauli ya
Bindeshwar Pathak, mvumbuzi wa vyoo hivyo nafuu.
0 comments:
Chapisha Maoni