Watu wanane wanashikiliwa na polisi wakiwemo
Madaktari kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio l a kutupwa kwa mabaki ya
miili ya binadamu jana jioni nje kidogo ya jiji la Dsm
Huku likiendelea na uchunguzi kuhusu tukio
hilo,Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova
ametangaza kuundwa kwa jopo la upelelezi kuchunguza tukio hilo, ili
kubaini taratibu gani zilikiukwa na kujua aina ya mashtaka
itakayowakabili.
Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa miili hiyo
ilikua katika Taasisi ya mafunzo ya udaktari IMTU kabla ya kukutwa
imetupwa eneo la Bunju.
Taasisi hiyo imekiri kwamba mabaki ya miili ilikua katika taasisi hiyo lakini haijatoa maelezo kuhusu kutupwa kwa miili hiyo.
Kamanda Kova amewatoa wasiwasi watanzania kuwa
hakuna mauaji yoyote ya kimbari yaliyotokea sehemu yeyote nchini hivyo
polisi iachiwe ifanye kazi yake kisha itatoa taarifa hapo baadae.
0 comments:
Chapisha Maoni