MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga
klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amepata ofa nne
za kujiunga na klabu mbalimbali barani Ulaya.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Samatta
alisema nchi karibu nne zimemfuata na kuonyesha nia ya kumtaka, lakini
bado anatafakari.
Samatta nyota aliyetimkia Mazembe akitokea klabu ya Simba ya
Tanzania, alisema, tayari ameshautaarifu uongozi wake wa klabu yake juu
ya ofa hizo, lakini wasiwasi wake ni nafasi ya kuachiwa kwake na timu
hiyo ambayo bado ana mkataba nao wa msimu mmoja.
Timu hizo na nchi ziliko sitoweza kuzitaja kwa sasa, mambo yatakapokaa sawa nitaweka wazi kila kitu, si unajua tena. Lakini nina wasiwasi, sijui kama uongozi wa timu yangu watakubali niondoke kutokana na mchango wangu katika timu hiyo
alisema Samatta.
Aliongeza kuwa anawafahamu viongozi wake kuwa ni waelewa, hivyo basi
wakati ukifika anamuomba Mungu amtangulie ili aweze kuruhusiwa kwenda
kutimiza ndoto zake barani Ulaya.
0 comments:
Chapisha Maoni