Ijumaa, Julai 18, 2014

MADHARA YA KULALA NA NGUO ZA NDANI

Wataalam wa magonjwa ya kina mama na watoto wamebainisha madhara ambayo yanaweza kuwapata kina mama na wasichana wenye tabia ya kuvaa nguo za ndani wakati wa kulala, maumbile ya kike yanaitaji kupumua ili kuzuia maambukizi kama vile fangasi ndio maana madaktari wanashauri kulala bila nguo au kuvaa vinguo vyepesi.
Dr. Grace Obong, anasema ya kwamba wakati wa mchana wanawake pia huvaa chupi mbalimbali na nguo za kubana ambazo ufanya sehemu zao za siri kupumua kwa shida sana anaendelea kwa kusema kuwa ingawa inashauriwa wanawake kvaa material aina ya pamba lakini wanawake wengi hawapendelei kabisa aina hiyo ya nguo za ndani hivyo ni muhimu wakati wa kulala usiku kuacha maumbile yapumue vizuri.
Dr huyo anashauri kuvaa boxer pamoja na pajama baadhi ya magonjwa au maambukizi yatokanayo na kukiuka hayo hapo juu ni pamoja na Bacterial vaginosis Maumbile ya kike yameumbwa kuwa na bacteria ambapo hu balance bacteria wabaya ni wengi ukilinganisha na bacteria wazuri . Maambukizi yaitwayo Bacterial vaginosis hutokea pale mlingano huu unaposhindwa kubalansi. mwanamke mwenye maambukizi upata adha ya kutokwa na majimaji yenye harufu mbaya na pia wachache hulalamika kupata harufu ya shombo la samaki .Mara baada ya tendo la
ndoa majimaji hayo yanaweza kuwa na rangi ya maziwa au grey na dalili zngine ni kuungua wakati wa kukojoa magonjwa mengine ni kama yeast infection na mengine mengi.. Dr anamaliza kwa kusema ni muda wa kulala natural na kuepuka unyevu unyevu usiokuwa wa lazima huko chini

0 comments:

Chapisha Maoni