Arsenal wameanza tena kumfuatilia kiungo wa Bayer Leverkusen Lars
Bender, huku Arsene Wenger akiwa anakaribia kukamilisha usajili wa
Alexis Sanchez na beki Mathew Debuchy (Daily Telegraph), Arsenal
wamekubaliana na Barcelona pauni milioni 34 za kumsajili Sanchez, lakini
Barca bado wanatazama kama Juventus wanaweza wakatoa dau kubwa zaidi.
Liverpool pia wanamtaka Sanchez, lakini mchezaji huyo hataki kwenda
Anfield. Manchester United wameambiwa kuongeza dau
kama wanamtaka beki Daryl Janmaat kutoka Feyenoord (Metro), Luis Nani
atakuwa mtu muhimu wakati Man U wakimfuatilia Arturo Vidal wa Juventus
(Evening News), Southampton wanajiandaa kutoa pauni milioni 8 kumsajili
kipa wa Cardiff David Marshall (Daily Mail), Louis van Gaal anapanga
kutumia mkakati wa 3-4-3 anaotumia na Uholanzi wakati atakapoanza
kuifundisha Man U (Daily Mirror), Monaco wanamtaka kiungo wa Newcastle
Moussa Sissoko ambaye pia anasakwa na Liverpool (L'Equipe), Arsenal,
Tottenham, Napoli na Borussia Dortmund wote wanamwania kiungo wa
Southampton Morgan Schneiderlin (L'Equipe), Manchester United na Paris
St-Germain wapo tayari kutoa pauni milioni 47 kumsajili winga wa Real
Madrid Angel Di Maria (AS.com), Marouane Fellaini ambaye amekuwa na
wakati mgumu Man U huenda akachukuliwa na Fiorentina (Lefigaro), Monaco
wamewaambia Real Madrid kutoa pauni milioni 63 kama wanamtaka kiungo
kutoka Colombia James Rodrigues (AS.com), mmiliki wa AC Milan Silvio
Berlusconi ana wasiwasi kuwa hatopata bei anayotaka kwa Mario Balotelli
kwa Arsenal kutokana na kutofanya vyema katika Kombe la Dunia. Tetesi
nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!!
0 comments:
Chapisha Maoni