Siku kama ya leo miaka 126 iliyopita John Boyd Dunlop raia wa Uingereza,
alikuwa mvumbuzi wa kwanza wa gurudumu. Dunlop alifikia hatua ya
kuvumbua gurudumu la magari baada ya kupita miaka kadhaa ya utafiti.
Alifariki dunia 1921.
Siku kama ya leo miaka 60 iliyopita, inayosadifiana
na tarehe 21 Julai 1954 ulitiwa saini mwishoni mwa mkutano wa Geneva
mkataba wa kuacha vita kati ya Ufaransa na Vietnam na kukomesha ukoloni
wa Ufaransa huko India na China. Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya
kuanguka ngome imara ya Wafaransa iliyojulikana kwa jina la Dien Bien
Phu nchini Vietnam Mei mwaka 1954. Makubaliano ya mkutano wa kimataifa
wa Geneva, yalihudhuriwa na wawakilishi wa ngazi za juu kutoka Ufaransa,
Marekani, Uingereza, China, Vietnam na Urusi ya zamani. Kwa mujibu wa
makubaliano hayo, vikosi vya kigeni vilipaswa kuondoka Vietnam, lakini
Marekani kinyume na makubaliano ya Geneva, iliamua kutuma majeshi katika
eneo hilo kwa lengo la kuzuia kuungana maeneo mawili ya Vietnam ya
kaskazini na kusini.
0 comments:
Chapisha Maoni