Habari kutoka hospitali katika Kaunti ya Mombasa nchini Kenya zinasema kuwa,
watu wanne wameuawa baada ya kundi lililokuwa na silaha kufyatua risasi
katika eneo la Soweto, Likoni Kaunti ya Mombasa. Robert Kitur Kamanda wa
Polisi wa Kaunti ya Mombasa hakueleza kama shambulio hilo ni la
kigaidi au la uhalifu, bali alisisitiza kwamba watu wawili wameuawa
kwenye shambulio hilo lililofanywa na watu wenye silaha waliokuwa
wamepanda pikipiki. Hata hivyo, duru za hospitali kuu ya Mombasa
zinaeleza kuwa, viwiliwili vinne vililetwa hospitalini hapo kufuatia
shambulio hilo la jana. Duru hizo zimeeleza kuwa, watu wengine wanane
walijeruhiwa kwenye shambulio hilo. Kamanda Kitur amesema kuwa, hakuna
kundi lolote lililotangaza hadi sasa kuhusika na shambulio hilo.
Mashuhuda wa tukio hilo katika eneo la Soweto wanasema kuwa, watu wanne
wenye silaha walitekeleza shambulio hilo lililochukua muda wa dakika
kumi na tano.
0 comments:
Chapisha Maoni