Jumanne, Julai 01, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Siku kama ya leo miaka 54 iliyopita, sehemu mbili za Somalia ya Uingereza na ya Italia ziliungana na kuunda nchi moja ya Somalia yenye kujitawala. Karne kadhaa nyuma, Somalia iliwahi kujitawala kwa kipindi kifupi. Mwaka 1884 Uingereza iliiweka katika himaya yake sehemu ya ardhi ya nchi hiyo. Miaka mitano baadaye Italia nayo ikakoloni baadhi ya sehemu za Somalia. Harakati za mapambano za Muhammad Abdullah Hassan dhidi ya Waingereza kuanzia mwaka 1901 hadi 1920 hazikusaidia kitu. Mwaka 1950 Umoja wa Mataifa uliitaka Italia iandae mazingira ya kujitawala na kuwa huru Somalia.
Miaka 52 iliyopita katika siku kama hii ya leo, Rwanda ilipata uhuru. Rwanda ina historia inayofanana na jirani yake wa kusini yaani Burundi ambapo kabla ya nchi hizo kujitangazia uhuru zilikuwa zikikoloniwa na Ubelgiji. Mwaka 1973, Meja-Generali Juvenal Habyarimana alichukua madarakani baada ya kufanya mapinduzi yasiyo ya umwagaji damu. Baada ya mapambano mtawalia ya wapigania uhuru wa Rwanda, hatimaye mnamo mwaka 1962, nchi hiyo ilipata uhuru na kabila kubwa la Wahutu likashika hatamu za uongozi wa nchi. Hata hivyo mwaka 1994 kulitokea mauaji ya kimbari ambapo zaidi ya watu laki 8 waliuawa wengi wao wakiwa ni wa kabila la Kitutsi.
Siku hiyo hiyo ya tarehe Mosi Julai pia nchi jirani ya Burundi ilipata uhuru.
Na siku kama ya leo miaka 1022 ilyopita inayosadifiana na tarehe 3 Ramadhani 413 Hijria, alifariki dunia Muhammad bin Nu'uman maarufu kwa lakabu ya Sheikh Mufiid, faqihi, mtaalamu wa elimu ya hadithi, Qurani Tukufu na historia ya Kiislamu. Sheikh Mufid alikuwa hodari na mwanafikra aliyepevuka, kwani aliweza kujibu masuala ya kifiqihi kwenye midahalo kulingana na madhehebu yoyote aliyotakiwa kufanya hivyo. Kutokana na uhodari wake huo, maulamaa wengi wa Kiislamu katika zama hizo walimpa lakabu ya Mufiid. Sheikh Mufiid ameandika vitabu vingi miongoni mwa hivyo, ni al Kalaam Fii Dalaailil Quran', al Arkaan' na˜Kashful Saraair'.

0 comments:

Chapisha Maoni