Liverpool imesema haikuhusika na chochote
kuhusiana na hatua ya kuomba radhi ya Luis Suarez baada ya kumng'ata
Giorgio Chiellini, ili kusaidia uhamisho wake kwenda Barcelona
(Independent), Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anapanga kutoa pauni
milioni 23 kumchukua kiungo wa Real Madrid Sami Khedira ili kumsaidia
Mesut Ozil (Sun), Atletico Madrid wanajiandaa kutoa pauni milioni 20
kumchukua mshambuliaji wa Manchester City Alvaro Negredo (Daily Star),
Manchester City wanamtaka kipa wa Malaga
Willy Caballero ili kutoa ushindani kwa Joe Hart (Daily Mail), Arsenal
na Liverpool wanamfuatilia kwa karibu kipwa wa Costa Rica Keylor Navas
anayechezea Lavante, lakini ana kifungu cha kuzuia ununuzi cha pauni
milioni 6.5 (Daily Mirror), Tottenham wanapambana na Arsenal kumsaka
beki wa kulia wa Toulouse Serge Aurier raia wa Ivory Coast (Daily Mail),
Kiungo wa Chile Arturo Vidal amedokeza kuwa angependa kwenda Old
Trafford kuliko klabu nyingine (Daily Star), Mshambuliaji wa Chile,
Alexis Sanches anataka kusalia Barcelona msimu ujao, lakini inadaiwa
angependa kwenda Arsenal au Liverpool iwapo atalazimishwa kuondoka
(Metro), Beki wa kushoto wa Brazil Filipe Luis anataka sana kwenda
Chelsea kiasi kwamba amekata mawasiliano yote na klabu yake ya Atletico
Madrid (Daily Express), Arsenal wamekataliwa ombi lao kuhusu kiungo wa
Roma Alessandro Florenzi (Metro). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni