Baada ya Victoria Kimani kulalamika kuwa Ommy Dimpoz hakumuonyesha ushirikiano katika shooting ya
video yake inayofanyika hapa nchini, Ommy Dimpoz aongea upande wake.
Kiukweli ninachoweza kusema ni kwamba, habari hizo hata mimi zimenishtusha kwasababu nimeweza ku participate tangu mwanzo, na sidhani kama kuna tatizo na watu watarajie kuniona kwenye hiyo video.
Hakukua na tatizo lolote na mimi wala sina tatizo la kushoot na Director wa hiyo video, kwasababu mimi siwezi kumpangia Victoria mtu gani wa kushoot nae, mwisho wa siku mi nimeshirikishwa tu wala sio kusema nina mamlaka nayo ya kuamua, na kikubwa sina tatizo na sasa hivi tumewasiliana hapa nilikuwa naelekea location kushoot kwahiyo sijui ilikuwaje hata mimi mwenyewe nataka nionane nae nimuulize kitu gani hasa kimetokea.






0 comments:
Chapisha Maoni