Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘ameingizwa mjini’ na mhariri wa
filamu Bongo mwenye asili ya Kiarabu aliyejulikana kwa jina moja la
Chidy kwa kuingia mitini na shilingi 5,000,000 alizompa ili azihariri
filamu zake mbili lakini kazi haikufanyika.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania Kituo
Kikuu jijini Dar es Salaam, kilisema ilikuwa mwaka jana (2013) ambapo
Wema alimkabidhi mhariri huyo filamu mbili, Super Star na Vian Unaspect.
Ikazidi kudaiwa kwamba mbali na
filamu hizo, Wema alimlipa jamaa shilingi 2,500,000 ili kuzihariri
(editing) filamu hizo ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuingia sokoni.
Habari zikazidi kudai kwamba,
baada ya kuudaka ‘mpunga’ huo jamaa huyo amekuwa akimzungusha Wema
kufanya kazi zake na kumkabidhi ili azipeleke sokoni ndipo wiki
iliyopita mlimbwende huyo akalazimika kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo
cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, alimsikia Wema akisema filamu zote
zimemteketezea shilingi milioni 70,000,000 mbali na hizo alizomlipa huyo
mhariri wa filamu ambazo zikiingizwa kwenye gharama nzima inafika
shilingi 75,000,000.
Habari zaidi zinasema kwamba kama filamu hizo zingehaririwa mwaka jana na kuingizwa sokoni, Wema angekunja mkobani kiasi cha shilingi 140,000,000 hivyo kurudisha gharama za kuandaa (75,000,000) na faida juu (65,000,000).
Kufuatia maelelezo hayo kutoka chanzo chetu, mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi lilimsaka mrembo huyo ili afunguke kuhusu kuwepo kwa madai hayo, alipopatikana na kuulizwa sakata zima hakuwa tayari kupepesa macho, akakiri.
Habari zaidi zinasema kwamba kama filamu hizo zingehaririwa mwaka jana na kuingizwa sokoni, Wema angekunja mkobani kiasi cha shilingi 140,000,000 hivyo kurudisha gharama za kuandaa (75,000,000) na faida juu (65,000,000).
Kufuatia maelelezo hayo kutoka chanzo chetu, mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi lilimsaka mrembo huyo ili afunguke kuhusu kuwepo kwa madai hayo, alipopatikana na kuulizwa sakata zima hakuwa tayari kupepesa macho, akakiri.
Alisema awali kijana huyo aliyemdhulumu alikuwa mfanyakazi wake
katika kampuni ‘mufilisi’ ya Endless Fame, cha ajabu toka ampatie hiyo
kazi ya kumtengenezea pamoja na kumkabidhi fedha amekuwa akimchenga toka
mwaka jana.
Mimi nashindwa hata kumuelewa ana dhumuni gani na hizo kazi zangu maana hapo ana kama shilingi milioni 140 zangu, kwa kuwa kila kazi nilikuwa nalipwa shilingi milioni 70, nilishafanya makubaliano na Kampuni za Proin Promotion na Steps kuwapa filamu zangu lakini yeye ananizungusha, toka kipindi kile sijaende China, nikimuuliza majibu yake siyaelewi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Wema aliendelea kulalamika mpaka kufikia hatua ya kumwaga chozi:
Juzi kati Mtitu alitaka nifanye naye kazi lakini akanikumbushia Filamu ya Super Star, kwamba hajaiona sokoni mpaka sasa, ndipo nikamuelezea, akasema hawezi kukubali niipoteze kirahisi, lazima nisimame kidete kuipata ndiyo nikaenda naye mpaka Kituo cha Polisi Mabatini kufungua kesi na Chidy akakamatwa siku hiyo hiyo.
Wema aliendelea kusema:
Polisi walimpa siku saba ahahakikishe ananikabidhi kazi zangu pamoja na kompyuta moja ambayo aliichukua ofisini kwangu bila ridhaa ya mimi mwenyewe na akagoma kuirudisha.
Naye afisa mmoja wa polisi wa kituo hicho ambaye
alizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutoandika jina lake gazetini
alithibitisha Wema kufungua kesi Mabatini na ikapewa jalada Namba
KJN/RB/5850/14 WIZI WA KUAMINIWA 3/7/2014.
Ukweli ni kwamba zikipita siku saba bila kijana huyo kuleta fedha na kompyuta ya Wema hapa polisi, tutamsaka na tukimkamata sheria itachukua mkondo wake
alisema afisa huyo wa polisi.
Kama itakumbukwa sawasawa Filamu ya
Super Star ilizinduliwa Juni 24, 2012 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro
jijini Dar na nyota wa muvi za Nollywood (Nigeria), Omotola Jalade
Ekeinde alishiriki.




0 comments:
Chapisha Maoni