Timu ya taifa ya Arggentina imepokelewa kwa shangwe na maelfu ya watu
waliotaka kuwapongeza wachezaji wao, kuanzia uwanja wa ndege.
Wanandinga hao walishuka kutoka kwenye ndege maalum iliyokuwa
imenakshiwa kwa rangi za timu hiyo ikiwa na maandishi yaliyomaanisha
'Asante Argentina' kwa lugha ya kwao.
Wachezaji hao walipita kwenye
mitaa wakiwa ndani ya mabasi maalum huku kukiwa na mapokezi makubwa
kuwahi kushuhudiwa.
Argentina iliingia fainali za kombe la Dunia
2014, na kushindwa kutimiza ndoto yao ya kutwaa kombe hilo kwa kufungwa
na timu ya Ujerumani kwa bao moja.





0 comments:
Chapisha Maoni