Jumanne, Julai 15, 2014

RIHANNA ALIPOVUA NGUO KUISHANGILIA UJERUMANI

STAA wa Pop Rihanna usiku wa kuamkia jana aliungana na wachezaji wa Ujerumani kusherehekea ubingwa wao wa Kombe la Dunia baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina nchini Brazil.
Staa huyo aliyeonyesha mahaba dhahiri na timu hiyo ya Ujerumani akiwa ameshika jezi ya timu hiyo, alishindwa kuvumilia baada ya Mario Gotze kufunga bao katika dakika ya 113 ambapo aliamua kuvua nguo yake aliyokuwa amevaa na kuonyesha brazia yake.
Baada ya mtanange huo, Rihanna aliungana na wachezaji katika hafla ya kusherehekea ubingwa huo ambapo alipata fursa ya kupiga picha na wachezaji pamoja na kombe hilo.

0 comments:

Chapisha Maoni