Habari zinadai kwamba baadhi ya ndugu wa msanii wa Bongo Fleva, Nuh
Mziwanda ambao ni wakwe wa staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena
Mohamed ‘Shilole’ hawamtaki kwa madai kuwa ana umri mkubwa kuliko ndugu
yao.
Baadhi ya wanandugu hao (majina yanahifadhiwa) walisema umri wa Shilole siyo wa kuishi na ndugu yao, Mziwanda kwani hawaendani.
Ukweli ni kwamba mapenzi hayaingiliwi lakini tunaumia kuona ndugu yetu katika penzi zito na Shilole ambaye hawaendani kiumri
alidai mmoja wa
ndugu hao.
Alipotafutwa Shilole ili kufikishiwa ujumbe wa ndugu hao kwamba hawamtaki, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
0 comments:
Chapisha Maoni