Kigauni kifupi alichotinga staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper
Massawe katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa
Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kimeibua minong’ono
watu kuhoji kulikoni akivae hivyo ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Tukio hilo lilowastaajabisha wengi lilijiri wikiendi iliyopita katika
Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki, Dar ambapo asilimia kubwa ya
waalikwa katika hafla hiyo walisema hakikustaili hasa kwenye mwezi huu
wa toba.
Unajua siku zote tunaambiwa sisi Bongo Movie hatuna heshima, siyo kweli, kuna watu wapo kwa ajili ya kutudhalilisha. Angalia Wolper alichovaa
alisema mwigizaji mmoja ambaye hakutaka jina litajwe.
Alipoulizwa Wolper kuhusiana na madai hayo ya udhalilishaji, alijibu:
Achana nao hao ni wanafiki tu kwani kuna mtu amekatazwa kuvaa kama hivi?
0 comments:
Chapisha Maoni