Jumatatu, Julai 14, 2014

WAREMBO WA KIBONGO WAFUMANIANA CHINA, WAPIGANA NA KUVUANA NGUO MCHANA KWEUPE BARABARANI

Huku Waislamu wakiendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, warembo wawili, raia wa Tanzania (Wabongo), mmoja mkazi wa Sinza, Dar aliyetajwa kwa jina moja la Glory na mwingine ambaye jina halikupatikana, wanadaiwa kufumaniana laivu nchini China na kugeuka kituko cha aina yake.

Habari za awali zilidai kuwa Glory ndiye aliyemfuma mwenzake na bwana’ke, raia wa Nigeria kisha kumshushia kipigo kabla ya kutoana nje na kwenda kuchaniana nguo barabarani, mchana kweupe.
Akizungumza kwa njia ya simu, mwakilishi wetu toka nchini China (jina limehifadhiwa), alisema kuwa akiwa katika pitapita zake za kukusanya matukio ili kuyatuma Bongo kuonesha jinsi gani Wabongo wanavyoidhalilisha nchi yao ughaibuni, wikiendi iliyopita alitembelea eneo la Guangzhou Rujing Lu Sky Coffee nchini humo ambalo Watanzania wengi hufanyia ‘biashara’ zao.
Mwakilishi huyo akiwa eneo hilo linalosifika kwa matukio na starehe za kichumbani ndipo alipokumbana na timbwili hilo ambalo linaichafua taswira ya Wabongo ambao wanakwenda China kuchukua biashara mbalimbali.
Dah! Hii ni aibu kubwa ambayo sijawahi kutegemea kuwa nitakutana nayo, yaani Wabongo kwa Wabongo wanapigana, wanachaniana nguo na kuumizana kisa bwana wa Kinigeria, tena ughaibuni!
Alisema kwa masikitiko mwakilishi huyo nchini China.
Akiendelea kufunguka, alisema kwamba ilisemekana kuwa Mnigeria huyo aliwahi kuwa na uhusiano na Glory hivyo siku ya tukio, jamaa alimtosa Glory na ‘kuchepuka’ na mwenziye.

Ilielezwa kwamba Glory hakukubali ndipo akamuanzishia timbwili mwezake na kumpa kipigo cha mbwa mwizi akimtuhumu kwa nini amemchukulia bwana’ke.
Katika timbwili hilo, warembo hao walijikuta wakichaniana nguo na kubaki nusu utupu huku wakirushiana matusi ya nguoni (hayaandikiki mtandaoni kimaadili).
Wakati wakipigana waliingia barabarani na kusababisha bonge la foleni huku wakinusurika kukanyagwa na magari hasa walipoangushana katikati ya barabara.
Kuna wakati Glory alimkaba mwenzake hadi mashuhuda wa sinema hiyo ya bure wakahisi anamuua mwenzake hivyo kulazimika kuita polisi wa usalama barabarani ambaye alifika mara moja na kuwaamulia. Ilisemekana kwamba, askari huyo alipoona hawaelewani lugha ndipo akawaachia huku kila mmoja akichukua hamsini zake.
Baada ya kupata taarifa hizo,chanzo kilifanya jitihada za kumtafuta Glory kwa njia ya simu yake ya kiganjani lakini hakupokea na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kuhusiana na tukio hilo, licha ya kuonekana umemfikia (delivered) hakujibu hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.

0 comments:

Chapisha Maoni