Mwanafunzi wa darasa la sita
anayesoma shule ya msingi (jina linahifadhiwa kimaadili) amekutwa kwenye kambi
ya machangudoa akidaiwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza mwili.
Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita maeneo ya Kahumba mjini Morogoro
usiku wa manane ambapo chanzo kilipokea simu kutoka kwa watu
walioumizwa na jambo hilo huku wakimwonea huruma kwani alikuwa
akichukuliwa na mijibaba.
Chanzo kilipofika eneo la tukio kilimshuhudia binti huyo lakini ilipotaka
kuita polisi, wenzake waliokuwa wakijiuza naye walikuja juu wakitaka
kumshushia kipigo mwanahabari wetu.
Kesho yake Chanzo kilikwenda kumsaka mtoto huyo ambapo mama aliyejitambulisha kwa jina la Nasra Hamis Ndehere alikuwa miongoni mwa wazazi waliojitokeza baada ya kukerwa na tabia ya mtoto huyo ya kujiuza.
Kesho yake Chanzo kilikwenda kumsaka mtoto huyo ambapo mama aliyejitambulisha kwa jina la Nasra Hamis Ndehere alikuwa miongoni mwa wazazi waliojitokeza baada ya kukerwa na tabia ya mtoto huyo ya kujiuza.
Baada ya kumnasa, binti huyo alikiri kujihusisha na biashara hiyo haramu
kwa kisingizio cha ukali wa maisha baada ya kufiwa na wazazi wake,
alidai alikuwa akitafuta pesa ya kununulia nguo za Sikukuu ya Idd.
Pia mtoto huyo alidai kuwa nyumbani kwao ni Mwanza na alipoulizwa kama
anaweza kuwasiliana na ndugu zake alijibu anaweza hivyo alipewa simu ili
awapigie lakini namba zao hazikuwa hewani.
Baada ya kuona hali hiyo, chanzo kwa kushirikiana na mama huyo waliamua kumpeleka mtoto huyo Ustawi wa Jamii.
Katika hali ya kushangaza, wakati wanaelekea Ustawi wa Jamii, walikutana
na msichana ambaye baada ya kuwaona alisema binti huyo siku hizi
haonekani shuleni kwani anasoma naye darasa moja.
Kufuatia kauli hiyo, mama huyo alimshushia kichapo kikali denti huyo hivyo kujaza umati.
Baada ya kuona hali hiyo, chanzo kilijitosa kumnusuru denti huyo kwa kuita
polisi wa pikipiki ambao walifika fasta na kumpeleka mtoto huyo kituo
kidogo cha polisi Kata ya Mji Mpya mjini hapa ambapo alikabidhiwa kwenye
Dawati la Jinsia.



0 comments:
Chapisha Maoni