Uongozi wa kizazi kipya upo tayari kushika hatamu za uongozi na kuijenga
Tanzania mpya, kwa fikra mpya na maarifa mapya. Mabadiliko, kokote
yalikotokea, yalidaiwa na kuongozwa na vijana. Vijana wa Tanzania
washike usukani wa kuleta mabadiliko wanayoyataka. Ukiona kijana
anamwambia kijana mwenzake hana uzoefu, basi kazi ya kuleta mabadiliko
ni kubwa zaidi. Kutokuwa na uzoefu ni sifa ya kijana. Tusi kubwa kwa
Obama mwaka 2008 lilikuwa ni kukosa uzoefu, kukosa rekodi. Tusi hilo
lilikuwa muziki kwa wapiga kura wa Marekani. Tanzania mpya inahitaji
viongozi wapya, mazoea mapya, fikra mpya na maarifa mapya. Inahitaji
kuthubutu mambo makubwa sio kulinda uzoefu wa nyuma. Tunaweza.
0 comments:
Chapisha Maoni