Jumatatu, Julai 28, 2014

DULLY SYKES AELEZEA UKAME WA SHOW KWA UPANDE WAKE

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, amesema ni miaka miwili sasa hajapigiwa simu na promota yeyote nchini kwa ajili ya kufanya shoo.
Dully amesema hiyo imetokana na yeye kutojiweka sokoni, akifanya kazi za utayarishaji wa muziki huo.
Alisema hawezi kufanya shoo kwa bei ambayo yeye haitaki kwani amejiwekea kuwa hawezi kufanya shoo ya chini ya sh. mil. 10.
Shoo zangu nyingi sifanyi chini ya milioni 10, hivyo anayenihitaji ajue nataka nini sio kuniita kwa bei za mtaani na kupotezeana muda, kila msanii ana malengo yake
alisema.
Dully aliyetamba na vibao kadhaa kama ‘Salome’, ‘Mtoto wa Kariakoo’, ‘Dhahabu’ na nyinginezo nyingi, yu miongoni mwa wasanii mahiri nchini.

0 comments:

Chapisha Maoni