Jumatatu, Julai 28, 2014

AJALI NYINGINE YA NDEGE MAREKANI, VIDRO IKO HAPA

Sasa tukio jingine la saa kadhaa zilizopita ni kuhusu ndege ndogo ya abiria ambayo imelazimika kutua kwa dharura ufukweni huko Venice Florida Marekani baada ya kupata tatizo ikiwa angani na rubani kuona hakukuwa na uwezekano wa kufika uwanja wa ndege alikofanya mawasiliano.
Kutua huku kwa dharura kumesababisha kifo cha Mwanaume mmoja alikua akitembea ufukweni huku mtoto wake wa kike akijeruhiwa vibaya kwenye hii ajali.
Rubani na abiria wake hawakuumia kwenye hii ajali ila mtoto wa kike ambae anahisiwa kuwa na umri wa miaka 10 ndio ameumia sana na kukimbizwa hospitali.

0 comments:

Chapisha Maoni