Jumatatu, Julai 28, 2014

JAMES RODRIGUES NI ZAIDI YA RONALDO MADRID

Klabu ya Real Madrid imeonyesha kutojutia gharama zilizotumika wakati wa usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Colombia James Rodriguez aliyesajiliwa juma lililopita akitokea kwenye klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa.
Real Madrid wamethibitisha kuanza kurejesha sehemu ya gharama za usajili wa mshambuliaji huyo baada ya kukiri kufanya mauzo ya jezi namba 10 ya Rodrigues kwa kiasi kikubwa.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo inaeleza kuwa, mpaka sasa jezi 345,000 za mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 zimeshanunuliwa na mashabiki wa mjini Madrid pamoja na sehemu mbali mbali ulimwenguni kote.
Mauzo yaliyofanyika yanafikia kiasi cha Euro million 33.4 ikiwa ni inakaribia nusu ya ada ya usajili iliyotumika katika uhamisho wa Rodrigues ambayo ilikuwa ni Euro million 80.
Mpaka taarifa hizi zinatolewa bado jezi ya Rodrigues ilikua inaongoza kwa mauzo, ambapo tathmini iliyofanyika inaonyesha kwa muda wa saa moja mashabiki hununua Jezi 1,000.
Tafiti zinaonyesha kuwa, mkoa wa Arusha unaongoza kwa kilimo haramu cha bangi ambayo imekuwa ikiharibu maisha ya vijana wengi licha ya viongozi wa mkoa huo kukemea vikali juu ya ustawishaji wa mmea huo huku wakisisitiza kula sahani moja na wahusika bila mafanikio, ambapo eneo la Kisimiri lililopo Wilayani Arumeru likitajwa kuongoza kwa kilimo hicho.
Aidha, kumekuwepo na mjadala katika mtandao wa JamiiForums kuwa Polisi mkoani humo baada ya kufanikiwa kwa kiasi fulani kunasa genge la ulipuaji mabomu, sasa limeelekeza nguvu zake katika suala la mihadarati hali iliyotajwa kuchangia kunaswa kwa magunia hayo.
- See more at: http://www.fikrapevu.com/shehena-ya-magunia-20-ya-bangi-yakamatwa-arushashehena-ya-maguni-20-ya-bangi-yakamatwa-arusha/#sthash.zvGpXqsD.dpuf

0 comments:

Chapisha Maoni