STUDIO ya Bongo Record iliyo chini ya mtayarishaji mkongwe nchini, P
Funk Majani, inatafuta wasanii wapya wenye vipaji ikiwa ni pamoja na
wale wanaojijua kama wana bahati.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Majani alisema anatafuta
wasanii watano ambao watafanya kazi chini ya lebo ya Bongo Record kwa
upade wa wanawake na wanaume.
Alisema anataka kuchanganya pamoja ili atengeneze kundi ambalo
atatangaza nia yake hapo baadae, kwa wasanii wa Bongo fleva, hip hop na
watayarishaji.
Hao wote watakuwa kwa lebo ya Bongo Record ambayo ilikuwepo zamani ikijengwa na wasanii mbalimbali, sasa hivi tumerudi tena kwa lengo la kukuza muziki wetu
alisema.
Majani alisema kwa yeyote ambaye anataka kuwa chini ya lebo hiyo anatakiwa kutuma kazi zake kwenye bongo_recordz@yahoo.com ili kumuwezesha zionekane.
0 comments:
Chapisha Maoni