Wanariadha wanaume wamekiri kuanza kunywa maziwa ya
Matiti kama njia ya kusisimua misuli yao badala ya kutumia madawa
yaliyoharamishwa ambayo yanaongeza nguvu mwili.
Kwa mujibu wa jarida la Mail kwenye mtandao ,
wanyanyua uzani wengi wameanza kutumia maziwa ya matiti kama njia ya
kujipatia nguvu.
Mwanariadha mmoja kutoka mjini New
York kwa jina Antony, aliambia jarida la NYMag.com kwamba hukutana na
wanariadha kadhaa ambao hunywa maziwa hayo ambayo wanasema ni mazuri na
yanawapa nguvu.
Maziwa haya hununuliwa kwenye maduka ya
mitandaoni ikiwemo mtandao ujulikanao kama 'Only the Breast and Human
Milk 4 Human Babies' kwa dola mbili na nusu.
Mwanariadha huyo anasema kuwa maziwa hayo humpa nguvu za ajabu.
Sababu ya wao kufanya hivyo , ni kujizuia
kutumia madawa ambayo yamepigwa marufuku kwani wanaamini kuwa maziwa ya
Matiti ni njia ya kiasili ya kuwapa nguvu.
Mwanariadha mmoja ambaye ni baba wa watoto wanne
Jason Nash, anasema alianza kunywa maziwa ya mkewe baada ya mtoto wao
wa kwanza kuzaliwa na akahisi kuwa ikiwa maziwa hayo ni mazuri kwa mtoto
basi pia ni mazuri kwa watu wazima.
Ananukuliwa akisema kuwa maziwa hayo yamemlinda kutokana na magonjwa miaka hii yote.
Wanaume kadhaa wamezungumzia kunywa maziwa ya Matiti kama njia ya kuwapa nguvu badala ya kutumia madawa ya kusisimua misuli.
Akijibu wakosoaji wake, wanaosema kuwa ni kitu cha ajabu na
kushangaza, Antony alisema,'' mimi siamini madawa ya kusisimua misuli na
ninataka vitu vya asili, ambavyo havina athari zozote mbaya kwa
mwili.''
Wanaume wengine ambao sio wanaridaha ingawa
wanakunywa maziwa ya Matit, wanasema kuwa maziwa hayo huwafanya
kujisikia kama walio na nguvu mno na wenye afya tele.
David,mwenye umri wa miaka 42, kutoka Brooklyn,
aliambia jarida hilo kuwa alianza kunywa maziwa ya matiti miaka mitatu
iliyopita. Alisema ilisabidia sana wakati alipokuwa anapokea matibabu ya
Saratani kwa kuwa alikuwa anahisi kutapika wakati wote alipokuwa
anapokea matibabu.
Pindi alipokunywa maziwa hayo hisia za kutapika wakati wote zilimtoka
Alisema maziwa hayo ambayo ni matamu , yalimsaidia sana.
0 comments:
Chapisha Maoni