Serikali ya nigeria imebatilisha amri yake ya awali
ya kupiga marufuku maandamano ya kutaka wasichana waliotekwa nyara
Nigeria kuachiliwa.
Wasichana hao zaidi ya miambili walitekwa nyara
na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram katika eneo la Chibok Kaskazini
mwa Nigeria.
Wanaharakati hao walienda mahakamani lei kupinga marufuku hiyo iliyokuwa imetolewa na polisi.
Hata hivyo wanaharakati hao wapewa onyo kujizuia na ghasia wakati wa maandamano hayo.
Afisa mkuu wa polisi amesema kuwa maandamano
hayo ambayo yamekuwa takifanywa karibu kila siku ni tisho kwa usalama wa
nchi na kwamba kuna hofu kuwa wapiganaji wa kiisilamu huenda wakapenya
na kuingia kwenye maandamano hayo.
Maandamano hayo yamekuwa yakifanyika
kuishinikiza serikali kuongeza kasi juhudi zake za kuwanusuru wasichana
hao waliotekwa nyara na Boko Haram zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
Kauli mbiu ya maandamano hayo ni ''Bring Back
Our Girls'' yaani turejesheeni watoto wetu, na waandamanaji wanasema
kuwa maandamano yao yamekuwa ya amani.
Kundi la kiisilamu la Boko Haram, limesema kuwa
liko tayari kuwaachilia wasichana hao ikiwa serikali nayo itawaachilia
wapiganaji wake wanaozuiliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni