Rapper D Knob alitengeneza historia nyingine kwenye muziki
wake baada video ya wimbo wake ‘Nishike Mkono’ kuoneshwa kupitia kituo
cha Channel O ikiwa ni video yake ya kwanza kuchezwa katika kituo hicho
tangu aanze Muziki.
D Knob amesema kuwa hatua hiyo
ilikuwa kubwa sana kwake kwa kuwa tangu mwanzo alikuwa anahangaika
kupeleka video zake lakini hazikuwa zinachezwa. Lakini video ya Nishike
Mkono ilimsurprise baada ya kuona inamsogeza mbali licha ya kuitoa kwa
lengo la kuutambulisha tu ujio wake.
Tangu mwanzo nilikuwa natamani nyimbo zangu zichezwe Channel O.nilikuwa najaribu process za kupeleka kule. Wananiambia ingia online jaribu kupeleka…nilipopeleka jamaa wakawa wanajibu nini, tutumie link, tutumie biography yako na nini…
Amesema D Knob.
Baada ya kupitia hatua zote alizofanya, D Knob anasema aligundua kuwa
uandishi mzuri wa profile yake kuhusu safari ya muziki wake ni kitu
ambacho kiliwavutia Channel O baada ya kumfahamu vizuri kimuziki kupitia
profile hiyo.
Nimekuja kushtukia profile ina matter mno..profile ya maisha yako ya muziki. Unajua wale wanaposema tutumie profile wanataka kuangali wewe umefanya nini na wewe ni nani. Profile pia ndio inaeleza everything. Sasa ile profile pia inategemea unaiandikaje.
Ameeleza D Knob.
Ameeleza kuwa kitu kikubwa kilichomsaidia katika uandishi mzuri wa
profile yake ni kuwa wakati akiwa shule ilikuwa sehemu ya masomo yake.
Anasema wasanii wenzake wa karibu walikuwa wanashangaa kuona D Knob
anajibiwa na Channel O na kumpa maelezo wakati wao walituma na
hawajibiwi.
Washikaji wa karibu ambao nao wanatuma video zao wakawa wanashangaa wewe mbona wanakuelekeza sana. Kwa hiyo mimi nimekuja kujifunza kwamba inabidi mtu awe na profile ambayo imeandikwa vizuri. Profile ndio everything…unajua sio kila sehemu ambayo unaweza kutia maguu na kujieleza ‘mimi ni D Knob’, lakini unaweza ukamtumia tu mtu halafu wewe ukalala halafu baadae huyo mtu akakutafuta.
0 comments:
Chapisha Maoni