Ni swali aliloulizwa Spika mstaafu, Pius Msekwa katika mahojiano maalumu...
Akijibu swali hilo, Msekwa alieleza kwa ufupi
sababu za wasomi kuacha taaluma zao na kuwekeza nguvu na akili zao
katika siasa akisema inalipa kwa haraka na kwa njia nyingi zikiwamo
mishahara minono, posho na marupurupu kuliko zilivyo taaluma nyingine.
Msekwa ambaye amewahi kuwa Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, akitokea kwenye Chama cha Tanu na baadaye
kurejea kwenye siasa, alisema malipo manono yamewafanya wasomi wengi,
wakiwamo maprofesa, madaktari na wengineo kuifanya kimbilio.
Alisema pia uhuru wa watu kuchagua kazi nyepesi za
kufanya katika maisha yao umefanya waione siasa kama kimbilio rahisi
kuliko kutoka jasho kwenye taaluma, zikiwamo za utafiti, tiba, upasuaji,
ualimu na nyinginezo.
0 comments:
Chapisha Maoni