Kasisi mwandamizi wa kanisa Katoliki nchini Australia, Max Davis,
amejiuzulu baada ya kufikishwa kortini kujibu tuhuma za kuwalawiti
watoto wadogo. Imedaiwa kuwa, Max Davis alimlawiti mwanafunzi aliyekuwa
na umri wa miaka 13 katika chuo cha Saint Benedict mwaka 1969. Kasisi
huyo amekanusha tuhuma hizo na kusisitiza kuwa hajawahi kuhusika na uozo
huo.
Kashfa za makasisi wa Kikatoliki kuwadhalilisha kingono watoto wadogo
imezusha mpasuko mkubwa kwenye kanisa hilo huku baadhi ya ripoti
zikionyesha kuwa, makao makuu ya kanisa hilo (Vatican) imekuwa ikificha
makusudi uozo huo ili kulinda heshima yake. Mwaka uliopita, Kadinali
mwandamizi wa Australia alikiri kwamba, ofisi yake imekuwa ikiwakingia
kifua makasisi waovu kwa hofu ya kusambaratika kanisa hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni