Jumatatu, Juni 30, 2014

HIKI NDIO KIBURI CHA MAGUFURI

Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli, amesema itakuwa ni ndoto kwa vyama vya upinzani nchini kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM) iwapo wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri wataendelea kuwapo kwenye nafasi zao, akisema kuwa viongozi hao ni makada wa chama hicho tawala.
Alikuwa akizungumza jana na wananchi wa wilaya ya Chato kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi ya mabasi, huku akisema CCM kitaendelea kutawala milele kwa kuwa kina mizizi ya kutosha.
Ndugu zangu wananchi, niwahakikishieni kuwa CCM kitaendelea kutawala milele... hatuwezi kushindwa wakati wakuu wa wilaya ni wa CCM, wakurugenzi wote ni CCM, madiwani wengi nchini ni CCM, wenyeviti wa vijiji wengi ni CCM, wenyeviti wa vitongoji wengi ni CCM... wote hao mpaka kuja kuwaondoa madarakani siyo kazi rahisi
alisema Magufuli.

0 comments:

Chapisha Maoni