Uingereza inakabiliwa na upungufu wa Mbegu za kiume
hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki za matibabu ya uzazi nchini humo
kuchukua mbegu duni.
Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.
Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.
Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan
Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya
matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.
Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.
Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na
kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni
sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi
walipendelea kuficha majina yao.
Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi
kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume
wengi kutafuta watoto wao wenyewe.
Hatahivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiume bado upo.
Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa
binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka
katika mataifa ya kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.
0 comments:
Chapisha Maoni