Jumamosi, Juni 28, 2014

HATA KWA HILI PIA WANAWAKE MMESHTUKIWA

Kadri Mbinu zao zinavyozidi kujulikana ndivyo na wao wanavyobadili mbinu na kuja na New Models za kufikisha Ujumbe
 WANAITWA WANAWAKE
Ile style yao ya Bebi naomba Laki 3 nna shida ntakurudishia after 1 week ilifeli..Ikaja ya Baby naomba Laki 1 ya Saluni nayo ime-expire...SASA WANA MUPYAAAA,Bado inanukia Upya kama Telegram.
 Unakutana na demu,baada ya Wiki 2 anakwambia Birthday yake imekaribia na Hana Hela..Ukimuuliza lini Bday yako anakwambia This Weekend Baby..Unamwambia sawa.Ukizingatia ndo mmeanza-anza hata uvungu hujapewa,kila kitu unajibu Yes kama Questionnaire ya uchumba.
Profile yake ya Facebook inaonyesha Birthday yake ni November 22....Birthday aliyokupiga mzinga ni February 15..Sasa unajiuliza huyu mwenzetu ana Birthday 2 kwa Mwaka??
 Na ukimpa hiyo hela hata Birthday hutaalikwa,utaambiwa tu Baby,Ndo naenda kwenye Birthday tunafanyia huku kwa Bamkubwa huku Mbweni,tuko na shangazi yangu wa Hombolo na Wajomba zangu wale wa Ihumwa wamekuja...Ukitajiwa Bamkubwa hutakuwa na hamu hata ya kwenda.MZINGA SUCCESSFUL.
 Na huo mzinga wa Birthday anakuwa kawatumia MSG Wanaume kama 20 hivi,10 wakimpa hata utwente flani,tayari ana laki 2,unashangaa demu hana kazi,ndo anasubiria majibu ya Form 6 lakini ana Note 3 mpya,we unakazana kunyonga tai kurukia DCM za Keko deile na kikwapa juu na mshahara wako wa benki una Nokia Asha button zimechokaaaaaa
ENDELEENI KUTUKOMESHA....Demu una Birthday 3 kwa mwaka?mi nakuchora tu,au mwenzetu ulizaliwa kwa mafungu,February Kichwa...June Kiwiliwili...November Miguu"

0 comments:

Chapisha Maoni