Serikali imepandisha maradufu ada kwa wanafunzi wanaosomea ualimu kwenye vyuo vya ualimu nchini kuanzia muhula ujao wa masomo.
Ada hizo kwa wale wa ngazi za cheti na stashahada
ambazo zimeongezwa kwa karibu mara mbili au zaidi ya zile zilizokuwa
zikilipwa awali. Uamuzi huo ambao huenda ukawaathiri zaidi wanafunzi
ambao waliona ualimu kama kimbilio, unaelezwa na baadhi ya wadau
wakiwamo walimu, wanafunzi na hata wakufunzi wa baadhi ya vyuo nchini
kuwa ni wa ghafla.
Kwa mujibu wa baadhi ya wakufunzi, uamuzi huo
umetolewa kupitia waraka wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na
unatarajiwa kuanza kutekelezwa muhula wa pili wa masomo utakaoanza Julai
2, mwaka huu.
Kabla ya kupandishwa kwa ada hizo, wanafunzi
wanaosomea ualimu kwa ngazi ya cheti walikuwa wakilipa Sh200,000, lakini
sasa watalazimika kulipa Sh300,000, ikiwa ni ongezeko la asilimia 50.
Kwa wale wanaochukua stashahada watalazimika
kulipa Sh400,000 kwa masomo ya Sanaa na Sh600,000 kwa masomo ya Sayansi
kutoka Sh200, 000 za awali.
0 comments:
Chapisha Maoni