Mawakili wa mwanamke mkristo nchini Sudan ,Meriam
Ibrahim wamesema kuwa watawasilisha ombi mahakamani la kutaka mashtaka
ya kughushi stakhabadhi bandia dhidi ya mteja wao kuondolewa.
Bi Ibrahim alikamatwa siku ya jumanne,siku ambayo mahakama ya rufaa ilibadilisha hukumu yake ya kifo hadi kuwa ya uasi.
Kufuatia uamuzi huo alijaribu kutoroka nchini
humo kupitia stakhadhi za Sudan Kusini lakini akakamatwa katika uwanja
wa ndege wa Khartoum.
Wakili mmoja amekiambia kitengo cha habari cha
Ufaransa kwamba ana matumaini mamlaka itamuondolea mashtaka hayo na
kumpatia paspoti ya Sudan ili kumruhusu kuelekea nchini Marekani.
0 comments:
Chapisha Maoni