Wakati mamilioni ya fedha za Watanzania yakipotea kila mwaka
kutokana na ufisadi na misamaha ya kodi, imebainika kuwa baadhi ya
magereza nchini hayafai kutumiwa na wafungwa kutokana na kukosa sifa
ukiwemo uchakavu wa majengo.
Ripoti ya utafiti uliofanywa na Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora kwenye magereza na vituo vya polisi 102 katika
mikoa 12, inaeleza kuwa magereza 12 hayafai kutumiwa na binadamu.
Hali hiyo inaamanisha kwamba magereza hayo siyo tu
ni hatari kwa wafungwa na mahabusu, bali pia kiwa watumishi wa Idara ya
Magereza. Ripoti hiyo inaweka bayana kuwa magereza hayo yana hali mbaya
kutokana na majengo yake kujengwa miaka mingi iliyopita, huku mengine
yakikabiliwa na ukosefu wa mwanga wa kutosha.
Magereza yaliyotajwa kukosa sifa za kutumiwa na
binadamu ni Rombo, Nzega, Geita, Ngudu, Kasungamile, Ukerewe, Mugumu,
Musoma, Bunda, Ushora, Mang’ola na Bariadi.
0 comments:
Chapisha Maoni