KICHUPA (video) kipya cha mwanamuziki wa Tanzania Diamond
Platnumz, alichorekodia London, Uingereza, kimemgharimu zaidi ya Sh70
milioni kutayarisha licha ya audio ya wimbo huo kutengenezewa Nigeria
miezi miwili iliyopita.
Mteule huyo wa tuzo za BET ambaye amemshirikisha
mwanamuziki Iyanya kutoka Nigeria katika wimbo huo, amesema video hiyo
imemgharimu fedha nyingi, ambazo ameamua kuwekeza katika muziki huku
akiamini atavuna fedha nyingi kupitia muziki wake.
Diamond anasema anaumia sana pindi anapokuwa
akifanya kazi zake kwani huchukua kiasi kikubwa cha fedha na kuwekeza
katika muziki ili kukuza bongofleva na kuutangaza muziki wa Tanzania.
Si kwamba ninafanya hivi kama Diamond, la hasha! Bali ninafanya kwa mapenzi ya Tanzania. Lazima nihakikishe naendelea kuipeperusha bendera ya nchi yangu ili hata wageni wanaonijua sasa waone dogo sikubahatishaanasema Diamond.
Anasema alitumia Dola 25,000 pekee kumlipa prodyuza wa video hiyo, kwani alitakiwa amfuate London yalipo makazi yake.
0 comments:
Chapisha Maoni