Mtoto Nasra Rashid Mvungi (4), aliyefichwa
kwenye boksi kwa miaka minne, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) na katika saa zake za mwisho za uhai wake alisikika
akitamka maneno
sitaki waje kunichukua
Nasra ambaye alikuwa akitibiwa MNH, alifariki
dunia usiku wa kuamkia jana baada ya hali yake kubadilika Alhamisi
iliyopita, kiasi cha kuhamishiwa katika chumba cha uangalizi maalumu
(ICU) ambako aliwekewa mashine ya kumsaidia kupata hewa ya oksijeni.
Mama mlezi wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla
hajawa mahututi, mtoto huyo alikuwa akiweweseka kwa kuzungumza maneno
mengi hali iliyosababisha wauguzi kumfanyia ibada maalumu.
Sitaki waje kunichukua, sitaki, sitaki, wasije kunichukua, bibi Nasra umesikiani maneno aliyokariri mlezi huyo ambayo yalikuwa yakirudiwarudiwa na Nasra saa chache kabla ya hajawa mahututi na kupelekwa ICU.
Josephine alisema mtoto huyo pia kila mara alikuwa
akidai apewe chips na soda na kwamba hadi mauti yalipomkuta alikuwa
akitibiwa maradhi ya homa ya mapafu ‘nemonia’.
Nasra alifariki saa 7.30 usiku, tangu Alhamisi iliyopita hali yake ilibadilika na kuwa mbaya na imeendelea kuwa hivyo hadi alipofariki duniaalisema na kuongeza:
Bado niko Muhimbili nawasubiri watu wa ustawi wa Jamii kutoka Morogoro wao ndiyo watakuwa na uamuzi kuhusu mazishi ya mtoto huyoalisema.
Ofisa Habari wa MNH, Aminiel Eligaeshi
alithibitisha kifo cha mtoto huyo, ambaye alipokewa hospitalini hapo Mei
26 mwaka huu akitokea Morogoro na kwamba hali yake ilibadilika ghafla
juzi saa 2:00 usiku.
Jitihada za madaktari zilifikia kikomo saa 7:30 usiku, baada ya mtoto huyo kupoteza maishaalisema.
0 comments:
Chapisha Maoni