Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za
Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda
polisi mwenyewe kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye
umri wa miaka 17.
Faili la tuhuma dhidi ya Mbasha lilifunguliwa
Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati
shemejiye huyo (jina tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka
mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba
TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014.
Tangu siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa
inamsaka Mbasha bila ya mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa
huyo aliongea na gazeti hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na
kwamba yuko tayari kujisalimisha ili ukweli ubainike.
Tuhuma dhidi yangu ni za kutengenezaalisema Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia baina yake na Flora na familia yake ambao alisema umedumu kwa siku kadhaa.
Mimi sijabaka na sijawahi kubaka; sijatenda dhambi yoyote; sijafanya kitu chochote na kibaya haya mambo yote ni ya kusingiziwa tu. Mungu wangu ni shahidi. Na kwa kuwa sijafanya hiyo dhambi kama wanavyodai, basi Mungu wangu ataniteteaalisema Mbasha ambaye anaonekana zaidi kwenye video ya wimbo wa Maisha ya Ndoa alioshirikiana na mkewe Flora.
Si wamesema wananitafuta, nitakwenda mwenyewe polisi. Nitawasikiliza na nitatoa maelezo yangu. Kama wakinipeleka mahakamani basi ukweli utajulikana... ipo siku kila kitu kitakuwa wazi.
Kabla ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo,
msichana huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana)
ambako alifunguliwa faili la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo
ambavyo vilifanywa na daktari kung’amua kama binti huyo aliingiliwa
vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu utokaji wa mbegu usio wa kawaida
(HVD).
Kadhalika binti huyo alifanyiwa vipimo kuona kama
ameambukizwa virusi vya Ukimwi (VVU), pia kupata ujauzito, lakini
matokeo ya awali yalionyesha kuwa yupo salama.
0 comments:
Chapisha Maoni